Jumapili 26 Aprili 2026 - 23:30
Juhudi za kujenga upya Baqi‘ ziliongezeka

Hawza/ Kwa mnasaba wa kutimia miaka mia moja tangia kubomolewa kwa “Jannat al-Baqi‘”, kwa mara ya kwanza kongamano la kihistoria lililokusanya dini mbalimbali lilifanyika katika “Baraza la Bunge la Uingereza”. Katika mkutano huo, viongozi wa kidini na wasomi kutoka dini mbalimbali walisisitiza umuhimu wa kulinda urithi mtakatifu na kujenga upya kwa heshima Jannat al-Baqi‘, na wakalitaja suala hili kuwa ni la kibinadamu na kitamaduni lenye vipimo vya kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mnasaba wa kutimia miaka mia moja tangu kubomolewa kwa “Jannat al-Baqi‘”, kwa mara ya kwanza kongamano la kihistoria likijumuisha dini mbalimbali lilifanyika katika “Baraza la Bunge la Uingereza”. Katika mkutano huo, viongozi wa kidini na wasomi kutoka dini mbalimbali walisisitiza umuhimu wa kulinda urithi mtakatifu na kujengwa upya kwa heshima Jannat al-Baqi‘, na wakalitaja suala hili kuwa ni la kibinadamu na kitamaduni lenye vipimo vya kimataifa.

Kongamano hili liliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la al-Baqi‘ la Chicago na Taasisi ya al-Khoei ya London, na likafanyika chini ya uenyeji wa mbunge, Lord Russell Rook.
Katika mkutano huo, idadi ya viongozi mashuhuri wa kidini, wasomi na wawakilishi kutoka dini na madhehebu mbalimbali walihudhuria. Mkusanyiko huu ulionesha azma ya pamoja ya kulinda urithi mtakatifu na kuimarisha mshikamano wa dini tofauti.

Lord Rook katika hotuba yake ya ufunguzi, pamoja na kuwakaribisha wageni waheshimiwa, alisisitiza kwamba; kulinda urithi wa kihistoria na kidini ni jukumu la pamoja kwetu sote, na kufanikisha lengo hili hakuwezekani bila umoja na ushirikiano kati ya jamii mbalimbali.

Hujjat al-Islam Mahboub Mehdi Abedi Najafi, mwanachuoni wa Kihindi kwa niaba ya Shirika la al-Baqi‘, pamoja na kutoa shukrani kwa wenyeji na waliohudhuria, alieleza kwamba; madai ya kujenga upya Jannat al-Baqi‘ hayawahusu Waislamu pekee, bali ni suala la kimataifa linalohusiana na heshima ya mwanadamu, historia na maadili ya pamoja ya kibinadamu.

Hujjat al-Islam Ali Reza Rizvi, khatibu mashuhuri wa Kipakistani anayeishi London pia, alipongeza juhudi za Shirika la al-Baqi‘ na kusema: Viongozi wa dini na madhehebu yote wanapaswa kwa namna hii kusimama pamoja ili kuinua sauti ya pamoja kwa ajili ya haki na uadilifu duniani kote.

Miongoni mwa wazungumzaji waliohudhuria katika kongamano hili ni pamoja na Askofu Mkuu Anglos, Profesa Sajjad Rizvi (Chuo Kikuu cha Exeter), Padri Andrew Thomsen, Sara Lynn Cawti na Dada Aliyah A‘zam (mwakilishi wa Taasisi ya al-Khoei London).

Wazungumzaji katika hotuba zao walisisitiza umuhimu wa kulinda maeneo ya kihistoria na ya kidini duniani kote, na hasa umuhimu wa kujengwa upya Jannat al-Baqi‘ kwa namna ya heshima na hadhi. Suala hili liliwasilishwa katika muktadha wa urithi wa kitamaduni, haki za binadamu na ushirikiano wa kimataifa.

Hatimaye, mkusanyiko huu wa kihistoria ulimalizika kwa kusisitiza upya azma ya ushirikiano wa dini tofauti, mazungumzo yenye kujenga na kuunda jukwaa la kimataifa kwa ajili ya kulinda maeneo matakatifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha